Merz kukutana na viongozi wa Nordic kujadili ulinzi wa NATO
26 Mei 2025Miongoni mwa mada watakazojadili ni ulinzi wa Jumuiya ya NATO kuelekea kitisho cha Urusi pamoja na ushirikiano wa kiuchumi.
Tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake Ukraine, kitisho cha usalama kimeendelea kushamiri hasa kwa taifa la Finland linalopakana na Ukraine. Ripoti za wanajeshi wa Urusi kuwepo karibu na eneo la mpakani kati ya mataifa hayo pia imeendelea kuzidisha kitisho hicho cha usalama.
Mawaziri wa NATO wajadili sharti la uwekezaji wa ulinzi
Baadae jioni Friedrich Merz pia anatarajiwa kuhudhuria dhima ya chakula cha jioni hii leo na mawaziri wakuu wa mataifa hayo katika kasri la medieval katika mji wa pswani wa Turku Kusini Magharibi mwa Finland.
Finland na Sweden walijiunga na Jumuiya hiyo ya kujihami, NATO kufuatia Urusi kuanzisha uvamizi wake wa kijeshi Ukraine.