MigogoroUjerumani
Merz: Upo umuhimu wa kukubaliana haraka kuisaidia Ukraine
3 Machi 2025Matangazo
Akizungumza mjini Berlin leo, Merz amesema vyama nchini Ujerumani inafaa vijaribu kufikia mwafaka alau kabla ya mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika siku ya Alhamisi mjini Brussels.
Merz ambaye muungano wake wa kifadhina wa vyama ndugu vya CDU/CSU ulipata ushindi kwenye uchaguzi wa bunge wa mwezi uliopita hivi sasa ameanza majadiliano ya awali na chama cha Social Democratic (SPD) kuunda serikali mpya.
Amesisitita kwamba itakuwa busara ikiwa yeye na kansela anayeondoka madarakani Olaf Scholz watakuwa na msimamo wa pamoja kuhusu suala la nyongeza bajeti ya ulinzi na msaada kwa Ukraine hasa katika wakati Marekani imebadili mkondo kuhusu vita vya Ukraine.