Freiburg yashindwa kukamata nafasi ya nne kwenye Bundesliga
3 Machi 2025Matangazo
Freiburg iliingia mchezoni ikiwa na muendelezo mzuri wa matokeo baada ya ushindi wa mechi nne mfululizo lakini walizuiwa na safu imara ya ulinzi ya Ausgburg.
Freiburg ambao hawajawahi kucheza kandanda la Ligi ya Mabingwa Ulaya, wamemaliza wikiendi wakiwa katika nafasi ya tano, pointi moja nyuma ya nambari nne Mainz. Augsburg wameendeleza matokeo yao ya kutopoteza hadi mechi nane na sasa wako na pengo la pointi sita kutoka nafasi za kucheza Ulaya.
Mapema Jumapili, Holstein Kiel iliimarisha matumaini yao madogo ya kuepuka kushuka daraja kwa ushindi wa 1 - 0 ugenini didi ya washika mkia wenzao Union Berlin.