Fredrich Merz aahidi mageuzi Ujerumani
5 Mei 2025Matangazo
Kansela mtarajiwa nchini Ujerumani, Friedrich Merz, ameahidi kuleta mageuzi siku moja kabla ya kuapishwa kwake bungeni, kesho Jumanne kama Kansela na kiongozi wa serikali mpya ya mseto kati ya chama chake cha kihafidhina cha CDU na SPD.
Soma pia: Vyama vya CDU/CSU na SPD vyatia saini makubaliano ya kuunda serikali ya pamojaMuungano wa kihafidhina wa CDU/CSU ulioshinda uchaguzi mwezi Februari na viongozi wa SPD wamesaini mkataba wa kuunda serikali itakaiyoongoza Ujerumani kwa miaka minne ijayo.
Vyama hivyo vimeahidi kufufua uchumi wa Ujerumani, wakati ukishuhudiwa mgogoro wa kibiashara duniani ulioanzishwa na rais Donald Trump pamoja na kuimarisha bajeti ya ulinzi.