Fistula bado ni tatizo kubwa ulimwenguni
23 Mei 2025Kila mwaka, maelfu ya wanawake huathiriwa na fistula ya uzazi ambapo miongoni mwao wanapatikana katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inakadiriwa takriban wanawake 500,000 ulimwenguni, wanasumbuliwa na ugonjwa huo huku nusu yao wakiwa wanapatikana barani Afrika.
Kwa mujibu wa Hospitali ya Rufaa mjini kalemie, ugonjwa huo unapatikana haswa kwa kinamama waliopitia Ukatili wa kijinsia au wakati wa wakujifungua. Juditte Safi ni mtaalamu wa magonjwa ya wanawake katika Hospitali ya Rufaa mjini kalemie.
"Kuna watu ambao wamebakwa, wakati amebakwa anapata ugonjwa huo wa fistula. Njia nyingine ni wakati ambapo ana umri mdogo wakati wa kuzaa kwani kwenye taaluma yetu ya afya mwanamke anatakiwa kuzaa kuanzia miaka 20 na kuendelea. Mkojo huwa na saa yake ambayo inatoka, lakini mwanamke ambaye anajikuta mkojo unatoka wakati bila ya yeyekutaka lakini mkojo unatoka tunawaomba wale wamama waje hospitali ya rufaa na matunzo ni bure," Juditte Safi.
Uganda Kupambana na Ugonjwa wa Fistula
Ugonjwa huo huathiri wanawake kisaikolojia, wakati mwingine wanajikuta wakitengwa.
DW imesafiri Katika Kijiji Cha Kibanga umbali wa kilomita 15 kutoka kalemie, kumuona mama wa miaka 21, ambaye alipatwa na hali hiyo baada ya kujifungua mtoto wake akiwa chini ya miaka 20. Mama huyo hakutaka jina lake litajwe na pia sauti yake kusikika kutokana na kunyanyapaliwa, amesema kuwa
Unyanyapaa dhidi ya waathirika wa Fistula waongezeka
Mwanzoni hakujuwa kama ni ugonjwa, alinyanyapaliwa kwasababu ilikuwa vigumu kwake kuzuia mkojo na harufu mbaya, mumewe ndiye alikuwa msaada kwake. Mmewe ambaye tumempa jina la JUMA alikuwa na haya:
“Sio kazi rahisi kwasababu ndugu, jamaa na marafiki wananicheka na mke wangu, nilizani wamemloga mke wangu, kwasasa tunaishi maisha ya furaha kidogo na kuvumilia kwasababu baada ya waganga kunishauri nifuatilie matibabu ndipo naona afazali kidogo kwa mke wangu,” aliongeza kusema Juma.
Wagonjwa wa Fistula bado wakabiliwa na unyanyapaa
Daktari mkuu wa Hospitali ya Rufaa aliyejitambulisha kwa jina Moja la Mwamba amedai wanao hathirika wengi ni wale wanaoishi vijijini, hata hivyo amesema robo ya tatu ya mwaka Jana walipadua wamama 20 wenye fistula.
"Mimba Inaweza kuwa tayari ya kuzaliwa anakawia njiani, na inamletea matatizo kufika kwenye kituo Cha afya na baada ya kujifunguwa anashikwa na magonjwa ya fistula, mwaka Jana tulipasua wamama 20," ameongeza kusema daktari Mwamba.
Hospital hiyo inatarajia kutoa upasuaji kwa wamama wenye fistula mwezi ujao. Umoja wa Mataifa inatarajia kumaliza Fistula ulimwenguni ifikapo 2030.
Mwandishi: Zuberi Ally DW Kongo