FISCHER ZIARANI UTURUKI
25 Novemba 2003Matangazo
ANKARA: Waziri wa kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer amefanya ziara fupi mjini Ankara katika ishara ya mshikamano na Uturuki,kufuatia mashambulio ya mabomu yaliofanywa wiki iliyopita mjini Istanbul.Alipokutana na waziri mwenzake wa Uturuki Abdullah Gül,Fischer aliihimiza Uturuki iendelee na utaratibu wa mageuzi ulioanzishwa kama sehemu ya jitahada za nchi hiyo kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.Mashambulio manne ya mabomu yaliofanywa dhidi ya vituo vya Kiyahudi na Kingereza mjini Istanbul,yamesababisha vifo 53,na mia kadhaa wengine wamejeruhiwa.