FIFA yazindua ofisi ya kikanda nchini Morocco
27 Julai 2025Matangazo
Uzinduzi huo umefanyika wakati Morocco ikiendelea na maandalizi kwa ajili ya Kombe la Dunia la mwaka 2030 ambalo itakuwa mwenyeji pamoja na mataifa ya Uhispania na Ureno.
Rais wa FIFA Gianni Infantino alishuhudia sherehe hiyo ya uzinduzi na kusema siku hiyo itakumbukwa katika historia ya FIFA, kandanda ya Morocco, Afrika na dunia kwa ujumla. Ofisi nyingine za FIFA barani Afrika zinapatikana Senegal, Jamhuri ya Kongo, Rwanda na Afrika Kusini.
Uzinduzi huo, ulihudhuriwa pia na mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika, Patrice Motsepe, na ulifanyika saa chache kabla ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake 2025 huko Rabat, ambapo Nigeria ilijipatia ushindi wa mabao 3 kwa mawili dhidi ya Morocco.