Fidia kwa waathiriwa wa maandamano Kenya
27 Agosti 2025Jopo hilo linamjumuisha Profesa Makau Mutua ambaye ndiye mwenyekiti na mratibu mkuu, huku Faith Odhiambo Mony akiwa makamu mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa ni pamoja na Kennedy Ogeto, Irungu Houghton, Dkt. Linda Musumba na Juliet Chepkemei.
Kwa mujibu wa agizo la serikali, jopo hilo litaendesha kazi zake Hofu ya kuzuka ghasia Kenya yaibukakwa siku 120 kuanzia kuchapishwa kwake na linaweza kuongezewa muda iwapo haja italazimu. Kazi kuu ni kuandaa mfumo wa utekelezaji wa fidia utakaothibitisha na kugawanya malipo kwa waathiriwa, raia na maafisa wa usalama, waliouawa au kujeruhiwa kwenye maandamano na machafuko.
"Leo naanzisha na kuweka utaratibu wa muundo msingi wa kufidia wote waliopoteza maisha, waliojeruhiwa, waliolazwa kama sehemu ya kuliponya taifa letu.”
Katika kipindi cha miaka minane iliyopita, Kenya imekumbwa na misururu ya machafuko yanayohusiana na uchaguzi na maandamano ya kisiasa. Ripoti ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu inaonesha kuwa baada ya uchaguzi wa Agosti 2017, angalau watu 50 waliuawa wengi wao kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi ya polisi.
Ghasia za baada ya uchaguzi zasababisha mauaji ya watu wengi Kenya
Katika uchaguzi wa marudio wa Oktoba 2017, vurugu ziliendelea ambapo watu 17 waliripotiwa kufariki na zaidi ya 60 kujeruhiwa. Mnamo mwaka 2022, juhudi zakuwepo na uchaguzi tulivu nchini Kenya, uchaguzi ulifanyika kwa amani zaidi, lakini bado watu wasiopungua tisa walipoteza maisha katika maandamano yaliyofuata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya urais.
Maandamano ya mwaka 2023 na 2024, yaliyochochewa na kupanda kwa gharama ya maisha na misuguano ya kisiasa, yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 60 kwa jumla, huku zaidi ya 500 wakijeruhiwa. Njeri Mbugua alipoteza mwanaye kwa jina Daniel Mburu kwenye maandamano ya mwaka 2024, anapongeza hatua ya fidia.
"Tangu aage dunia ni mimi kujikaza sasa na hakuna mtu ametoka kwa barabara kujua kwa hivyo hiyo mambo ilinyamaza ndiyo leo tumesikia, deni alizoacha lazima zilipewa kwa hivyo kwetu ni ngumu.”
Kwa mara ya kwanza, Kenya hali ya wasi wasi yaendeleaserikali imeonyesha utayari wa wazi kushughulikia matokeo ya machafuko ya kisiasa kwa kulipa fidia na kuandaa mfumo wa haki unaojali utu wa raia. Hatua hii inaonekana kuwa mwanzo wa safari ndefu ya kujenga upya imani ya wananchi na kulinda uthabiti wa taifa.