Fidan asema Urusi na Ukraine zinataka vita visitishwe
30 Mei 2025Fidan ameyasema haya wakati akiwa ziarani mjini Kyiv kuelekea awamu ya pili ya mazungumzo ya ana kwa ana ambayo huenda yakafanyika kati ya pande hizo mbili mjini Istanbul wiki ijayo.
Ukraine bado haijathibitisha iwapo itatuma ujumbe katika mazungumzo hayo ambayo Urusi ilipendekeza yafanyike Jumatatu.
Ukraine kwanza inaitaka Urusi kuwasilisha mpango wake wa amani ambao Moscow imesema itauwasilisha tu, kwa ujumbe wa Ukraine watakapokutana katika mazungumzo hayo ya ana kwa ana.
Mapema wiki hii, Fidan alifanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.
Uturuki ambaye ni mwanachama wa NATO imekuwa mpatanishi muhimu wakati ambapo Rais wa Marekani DOnald Trump anashinikiza kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Haya yanafanyika wakati ambapo, maafisa mjini Kharkiv wanasema Urusi imefanya mashambulizi ya droni usiku wa kuamkia leo na kuwajeruhi watu kadhaa.