Morocco na Madagascar kukutana kwenye fainali CHAN
30 Agosti 2025Matangazo
Morocco wanalisaka kombe hilo ili waweke rekodi ya kuwa taifa lenye vikombe vingi katika michuano hiyo huku Madagascar wao wakitaka kuweka rekodi ya kulibeba taji hilo kwa mara ya kwanza.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa kumi na mbili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na utatanguliwa na sherehe mbalimbali za kufunga mashindano ambapo msanii Zuhura Otham au Zuchu wa Tanzania anatazamiwa kuwa miongoni mwa watumbuizaji.
Itakumbukwa kwamba michuano hii ya CHAN 2024 iliandaliwa kwa pamoja na nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.