Fainali ya CAF: Uwanja wa marudiano bado kitendawili
19 Mei 2025Sitofahamu inayoendelea kwa sasa ni wapi Mchezo huo utachezwa kwani Katika barua ya Caf iliyotumwa kwa Simba CAF walisema mchezo huo Utachezwa uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar huku Simba wao Mapema walitangaza mchezo wao utachezwa uwanja wa nyumbani Benjamin Mkapa.
Uwanja wa Benjamin Mkapa upo katika maboresho na katika taarifa iliyotolewa na maboresho yamefikia asilimia 85 na uwanja huu upo tayari kwa Fainali hiyo na Michezo mingine ya Kimataifa.
Katika mahojiano na Kaimu Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa Rashid Mijuza anasema"Hatuna shaka kabisa kuhusu maandalizi ya mchezo kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Eneo la kuchezea [Pitch] ambalo ndio lilikuwa na changamoto kwa sasa iko vizuri kabisa kwa upande wa Viti tumeshafunga viti Elfu 20000 kwa upande wa mifumo mingine kila kitu kwakweli kipo katika hali nzuri ya mchezo kuchezwa"Alisema Kaimu Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa Rashid Mijuza.
Je vipi kuhusu Mechi kuchezwa katika uwanja wa New Amaan Complex Kaimu Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa Rashid Mijuza anasema"Pengine labda tunaweza tukawa tumezidiwa katika nyanja za Fitina ya Mpira lakini kwa upande wa miundombinu sisi tuko vizuri kama kigezo ni eneo la kuchezea [Pitch] kwakweli sisi katika Pitch hatuna shaka yoyote"Alisema Kaimu Meneja wa uwanja wa Benjamin Mkapa Rashid Mijuza.
Athari ya uhakika wa uwanja utakaotumika
Sitofahamu ya Mechi ya Fainali kati ya Simba na Rs Berkane Uwanja wa New Amaan Complex wakati Wenyeji simba wanataka Mechi yao ichezwe uwanja wa Benjamin Mkapa inaweza kuwaathiri simba Kuelekea mchezo huu nimezungumza na Mchambuzi wa Soka Johanes Michael anasema'"Kwa asilimia kubwa inaweza ikawaathiri cha kwanza kwa mashabiki wao unajua Timu yoyote lazima itegemee Mashabiki na ukiangalia katika uwanja wa Benjamin Mkapa Simba imekuwa Tanuru lake analitumia Vizuri kupata matokeo lakini ukienda kwenye Uwanja wa New Amani Zanzibar Simba anaweza kuwa kama bado Mgeni na hii inaweza kuwa ni athari nyingine"Alisema Mchambuzi wa Soka Johanes Michael.
Lakini Naibu waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma "Sisi tunawasubiri CAF watuambie kwa sababu CAF walichoandika ilikuwa ni recomendation Ripoti yao mimi nimesoma wanasema Uwanja wa Benjamin Mkapa umekuwa na Measure improvemnt kwa hiyo sisi tumewapa ushahidi Sababu zilizotajwa za Kwanini mchezo huenda usichezwe Benjamin Mkapa ni dhaifu tumefanya kazi yetu inayotakiwa kufanyikwa na naamini CAF wataliona hilo na wataweka mchezo huu wa marudiano kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa"Alisema Naibu waziri wa Habari utamaduni sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma
Hadi sasa Simba hawajatoa Tarifa yoyote kuhusu Mechi yao itachezwa wapi huku machapisho mbalimbli katika mitandao ya kijamii yakihoji kwanini CAF Wachague mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Aman Zanzibar ambao unabeba mashabiki elfu 15000 tu Badala ya uwanja wa Benjamin Mkapa ambao unabeba Mashabiki Elfu 60000 ambao maboresho yameshakamilika.