Wataalamu wa lishe wanahimiza waumini wanaotekeleza ibada ya funga kuzingatia lishe bora wakati wa Iftar. Mtaalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Daktari Fredrick Mashil, anaeleza aina ya vyakula vinavyofaa kuzingatiwa wakati wa kufungua.