MichezoUswisi
Euro: Uswisi ina kibarua kigumu dhidi ya Uhispania
18 Julai 2025Matangazo
Uswisi, ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo, itakabiliana na Uhispania — mabingwa wa dunia — katika uwanja wa Wankdorf mjini Bern leo Ijumaa, wakiwa na matumaini ya kufuzu kwa mara ya kwanza katika nusu fainali ya mashindano hayo makubwa ya kimataifa.
Hata hivyo, Uswisi inakabiliwa na kibarua kigumu dhidi ya Uhispania, ambao walitia kimyani jumla ya mabao 14 katika mechi tatu za Kundi B. Hata hivyo Uswisi haina shinikizo kubwa la kushinda ikilinganishwa na wapinzani wao, ambao ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.
Mshindi wa leo atakutana na mshindi wa robo fainali ya pili kati ya Ufaransa au Ujerumani kwenye nusu fainaliitakayopigwa Zurich siku ya Jumatano ijayo.