EU na Israel zakubaliana kuboresha misaada kwa Wapalestina
10 Julai 2025Matangazo
Hatua hizo ni pamoja na kuongeza idadi ya malori ya kupeleka misaada na kufungua vituo na njia zinazotumika kwa ajli ya kusafirisha misaada.
Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa katika siku zijazo kwa maelewano kwamba misaada hiyo itapelekwa kwa wahitaji moja kwa moja ili kuepusha njama za kuipeleka misaada hiyo kwa wanamgambo wa kundi la Hamas.