EU kuwasaidia Wapalestina katika ujenzi mpya
14 Aprili 2025Umoja wa Ulaya umesema utasadia katika ujenzi mpya wa maeneo ya Wapalestina yaliyoharibiwa kutokana na mashambulizi ya Israel.
Umoja huo umeahidi kutowa dola bilioni 1.8 kwa kipindi cha miaka 3 ijayo. Taarifa ya halmashauri kuu ya Umoja huo imesema kwamba taasisi hiyo imejitolea kuwasaidia Wapalestina na iko tayari kuunga mkono amani endelevu na ya kudumu itakayozingatia kuundwa kwa madola mawili.Soma pia: Macron: Hamas haipaswi kuitawala Gaza baada ya vita
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametowa mwito wa kufanyika mageuzi katika mamlaka ya Wapalestina baada ya vita vya Gaza.
Macron pamoja na Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Wapalestina, waliozungumza kwa simu leo, wametowa mwito wa usitishaji vita haraka,na kuimarishwa kwa juhudi za kutowa msaada wa kibinadamu.