EU kufanya mazungumzo ya kibiashara na Marekani
14 Julai 2025Mkuu wa masuala ya biashara katika Umoja wa Ulaya Maros Sefcovic amesema anapanga kuwa na mazungumzo na wenzake wa Marekani leo Jumatatu, wakati Brussels ikipambana kukiondowa kitisho kipya cha ushuru wa asilimia 30 kilichowekwa na rais Donald Trump.
Sefcovic ambaye anayeziwakilisha nchi 27 za Umoja wa Ulaya katika mazungumzo na Marekani amesema Umoja huo utajaribu kufikia makubalianao mazuri ya kibiashara na mshirika wake Marekani lakini pia zinajiandaa kwa hatua za kukabiliana na ushuru waMarekani ikiwa mazungumzo yatashindikana.
Trump ameyatumbukiza mazungumzo hayo katika hali ya mashaka siku ya Jumamosi baada ya kutangaza kwamba ataweka ushuru wa ziada wa asilimia 30 dhidi ya Umoja wa Ulaya ikiwa makubaliano hayatofikiwa kufikia tarehe mosi August.