EU inatarajia kufikia makubaliano na Trump kabla Julai 9
7 Julai 2025Ametoa kauli hiyo baada ya kusema kwamba rais wa Halmashauri hiyo Ursula von der Leyen amekuwa na mazungumzo mazuri na Rais wa Marekani Donald Trump.
Haijawa wazi hata hivyo iwapo mazungumzo yao yamefikia hatua ya kutoiongezea Marekani Ushuru´ambaye ni mshirika mkubwa wa kibiashara barani Ulaya.
Zimesalia siku chache kabla ya kumalizika muda alioutoa Trump wa kufikia makubaliano na washirika wa kibiashara baada ya Kiongozi huyo wa Marekani kuanzisha vita hivyo vya kupandishiana ushuru ambavyo vimevuruga masoko ya dunia.
BRICS yasema haiko kuihujumu Marekani
Haya yanajiri wakati Rais Donald Trump akizishutumu nchi zinazofungamana na jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi BRICS kwamba mwelekeo wake ni wa kuipinga na kuihujumu Marekani na kutishia kuziwekea ushuru wa ziada.
Hata hivyo China kupitia msemaji wa wizara ya mambo ya nje Mao Ning imesema Jumuiya hiyo haitaki malumbano na Trump na kusisitiza kuwa hakuna mshindi katika vita vya kibiashara na kuongezeana ushuru.