Marufuku ya kuingia Ulaya yatolewa kwa washirika wa Assad
23 Juni 2025Matangazo
Watu hao wanadaiwa kuunga mkono uhalifu dhidi ya binaadamu, ikiwemo utumiaji wa silaha za kemikali kwa watu wa Syria na kuchochea mzozo wa kikabila.
Baraza la Umoja huo limesema marufuku hiyo iliwalenga maafisa watatu wa zamani wa jeshi la Syria lililohusika na ukiukwaji wa haki za binaadamu wakati wa utawala wa Assad, ukiwemo mateso na mauaji.
Marekani yaanza kuiondolea Syria vikwazo vya kiuchumi
Wengine ni wafanyabiashara wawili mashuhuri waliowakilisha biashara za serikali ya Assad na maslahi ya kifedha ya serikali hiyo nchini Urusi, ambayo Umoja wa Ulaya umesema zilisaidia kufadhili uhalifu huo dhidi ya binaadamu.