Ethiopia yawakamata makumi ya washukiwa wa kundi la IS
16 Julai 2025Kwa mujibu wa taarifa ya Huduma ya Idara ya Ujasusi ya Kitaifa, NISS iliyochapishwa na Fana,
washukiwa 82 walikuwa sehemu ya kundi hilo la IS linalohudumu katika jimbo linalojitawala la Puntland nchini Somalia.
Mashambulizi ya Marekani huko Somalia yawaua viongozi wa IS
Hapo jana jioni, Fana iliripoti kuwa NISS imekuwa ikifuatilia kwa karibu mikakati ya kundi hilo ya kupenyeza kwenye mipaka na juhudi zake za kuanzisha vikundi vya wanamgambovinavyoshambulia kwa maagizo nchini Ethiopia.
Kundi la IS nchini Somalia limezidi kuwa sehemu muhimu ya mtandao mkuu wa kimataifa wa wanamgambo katika miaka ya hivi karibuni.
Shambulio la Marekani lamlenga mpanga mikakati wa IS Somalia
Likiwa na takriban wapiganaji 700 hadi 1,500, tawi la IS nchini Somalia limeimarika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa wapiganaji wa kigeni pamoja na mapato.