Eritrea yataka Ethiopia iheshimu mipaka ya nchi yake
19 Machi 2025Serikali ya Eritrea imeitolea mwito jumuiya ya kimataifa wa kuishinikiza Ethiopia kuheshimu "uhuru na uadilifu wa mipaka ya majirani zake" wakati ambapo mvutano ukiongezeka kati ya mataifa hayo mawili ya Pembe ya Afrika.
Nchi hizo mbili ambazo zilikuwa maadui wakubwa tangu Ethiopia ipate uhuru wake mwaka 1993, zilitia saini mkataba wa amani mwaka 2018.
Soma: Kwa nini Ethiopia na Eritrea ziko ukingoni kuingia vitani?
Hata hivyo, baada ya vita vya Tigray mwaka 2020 hadi 2022, ambavyo Eritrea iliisaidia Ethiopia dhidi ya vikosi vya Tigray, uhusiano baina ya nchi hizo mbili ukadorora tena.
Malengo ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ya Ethiopia ya kupata ufikiaji wa baharini yameikasirisha Eritrea, ambayo inaishutumu kwa kutaka kuitumia bandari yake ya Assab.
Waziri wa habari wa Eritrea, Yemane Gebremeskel, amesema Eritrea inashangazwa na malengo potofu na yaliyopitwa na wakati ya Ethiopia ya kutaka kuwa na kambi ya jeshi la wanamaji 'kupitia diplomasia au nguvu za kijeshi.'