Uturuki iko tayari kuandaa mazungumzo ya Ukraine na Urusi
11 Mei 2025Uturuki imesema kuwa iko tayari kuwa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine. Hayo yamesemwa na Ofisi ya Rais Recep Tayyip Erdogan baada ya kiongozi huyo kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Katika mazungumzo hayo Erdogan amemwambia pia Putin kuwa kusitisha mapigano kutatoa mazingira yanayohitajika kwa ajili ya mazungumzo ya amani.
Soma zaidi: Erdogan kukutana tena na Putin kuhusu Ukraine
Mapema Jumapili, Putin alitoa pendekezo la mazungumzo ya ana kwa ana mjini Istanbul yanayolenga kuvimaliza vita kati ya Ukraine na Urusi. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amejibu kuhusu pendekezo hilo akisema nchi yake iko tayari kushiriki kwenye mazungumzo hayo Mei 15 kama Urusi itakubali kwanza kusimamisha vita.