Erdogan ataka chama cha PKK kuvunjwa mara moja
30 Machi 2025Katika hotuba yake ya siku kuu ya Eid ul Fitri inayoadhimishwa baada ya kukamilika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Erdogan amesema muda na uvumilivu kwa chama hicho unafika mwisho na kutaka kivunjwe mara moja huku akikitolea wito zaidi wa kuweka chini kikamilifu silaha zake.
Tarehe 27 mwezi Februari, kiongozi na muanzilishi wa chama hicho Abdullah Öcalan, aliyefungwa jela katika kisiwa kimoja nje ya Istanbul tangu mwaka 1999,alikitaka chama hicho kuweka chini silaha baada ya vita vya muda mrefu kati yao na serikali ya Uturuki. lakini chama hicho kimetoa masharti ya kutaka kwanza kiongozi wake kuachiwa huru kabla ya kutii amri.
Wito wa kiongozi wa PKK wapokelewa kwa furaha na mashaka nchini Uturuki
Uturuki imekataa masharti hayo ikiwa ni pamoja na tangazo la pamoja la kundi hilo la kusitisha mapigano.
Chama cha PKK, kilichotangazwa kuwa kundi la kigaidi na Umoja wa Ulaya na Marekani, kimeongoza uasi kwa miongo kadhaa dhidi ya serikali ya nchi hiyo tangu miaka ya 80.