SiasaSyria
Erdogan amsifu rais mpya wa Syria kwa kupambana na ugaidi
5 Februari 2025Matangazo
Akizungumza baada ya mkutano wao, Erdogan amesema amemuahidi al-Sharaa kwamba yuko tayari kumuunga mkono katika kupambana na ugaidi wa aina yoyote iwe ni kundi linalojiita Dola la Kiislamu au PKK.
Soma pia: Blinken asema raia wa Syria wanahitaji kulindwa
Uturuki imekuwa na mahusiano ya muda mrefu na Sharaa na ilimuunga mkono pakubwa waasi wa Kiislamu walipoanza kuweka shinikizo na hatimaye kumuondoa mamlakani Bashar al-Assad mnamo Disemba 8.
Sharaa alisafiri kuelekea Ankara kutoka Saudi Arabia ambako alitaka uungwaji mkono wa Saudia katika kuijenga upya Syria na kuufufua uchumi wake baada ya miaka 13 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.