Enrique: Ushindi wa Super Cup ni "muujiza"
14 Agosti 2025Licha ya ushindi huu kocha Enrique, amesema hawakustahili ushindi katika mechi hiyo kwani hawakufanya mazoezi ya kutosha ikilinganishwa na wapinzani wao.
Tottenham walionekana kuwa na dalili ya kumpa kocha wao mpya Thomas Frank ushindi wa kwanza, kabla ya mchezaji wa akiba wa PSG, Lee Kang-in, kufunga bao dakika ya 85, na Gonçalo Ramos kusawazisha kwa kichwa dakika ya nne ya muda wa nyongeza, na kufanya matokeo kuwa 2-2.
PSG walimiminika uwanjani kusherehekea, baada ya kuandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza ya Ufaransa kunyanyua kombe hilo.
Tottenham, waliomaliza nafasi ya 17 katika Ligi Kuu ya England msimu uliopita, mabao yakitiwa kimyani na Van de Ven na Cristian Romero dhidi ya PSG, ambao walitwaa Kombe la Ulaya kwa mara ya kwanza Mei kwa ushindi wa 5-0 dhidi ya Inter Milan.