Enrique: Ulikuwa muujiza kuishinda Super Cup
14 Agosti 2025Matangazo
"Sidhani kama tulistahili kushinda kutokana na tofauti ya muda ambao timu kama Tottenham ambayo imekuwa na muda mwingi wa kufanya mazoezi na sisi ambao tumefanya mazoezi kwa siku tano tu," alisema Enrique, "ni tofauti kwasababu nafikiri ni muujiza. Nina furaha kwasababu leo nimewaona mashabiki wetu kama kawaida yao wakiishabikia timu kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mechi."
Mabingwa hao wa Ulaya walilazimika kutoka chini mabao 2 ambapo walifunga la kwanza kupitia mchezaji wa akiba Kang-in Lee kunako dakika ya 85 halafu Goncalo Ramos akasawazisha katika muda wa ziada.
PSG waliishia kushinda kupitia mikwaju 4 ya penalti kwa 3 ya Spurs.