England yatinga nusu fainali michuano ya Ulaya ya wanawake
18 Julai 2025England imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Euro 2025 kwa Wanawake baada ya kutoka nyuma na kusawazisha mabao mawili na kisha kuifunga Sweden mabao 3-2 katika mikwaju ya penalti. Ushindi huo unaendeleza mbio za England za kutetea ubingwa wa michuano ya ulaya upande wa wanawake.UEFA wanawake yataka mechi zaidi kwenye viwanja vikubwa
Mabingwa hao watetezi wa Ulaya, walikuwa katika hati hati ya kuondolewa katika mashindano hayo wakati zikiwa zimesalia dakika 11 za muda wa kawaida kumalizika kabla ya kusawazisha mabao yote mawili katika dakika ya 79 na 81 ya mchezo.
England sasa itamenyana na Italia katika mchezo wa nusu fainali siku ya Jumanne. Italia wametinga nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997
Uhispania itakipiga leo na Uswisi huku Ufaransa ikiwa na miadi na Ujerumani kesho Jumamosi katika mechi mbili zilizosalia za robo fainali.