EL ALTO Rais mpya wa Bolivia akutana na viongozi wa waandamanaji
13 Juni 2005Matangazo
Rais mpya wa Bolivia, Eduardo Rodriguez, amekutana na viongozi wa waandamanaji wanaotishia kufanya maandamano mengine makubwa zaidi, iwapo hataahidi kutaifisha nishati ya gesi ya nchi hiyo.
Rodriguez, aliyechukua hatamu za uongozi Alhamisi iliyopita baada ya rais Carlos Mesa kujiuzulu kufuatia maandamano ya majuma matatu, amesema ataweza kuendelea mbele mara tu serikali mpya itakapokuwa tayari.