Duru ya tano ya mazungumzo ya Nyuklia kuanza Rome
22 Mei 2025Matangazo
Iran na Marekani zitakutana tena kwa duru ya tano ya mazungumzo mjini Roma kesho Ijumaa kuhusu mpango wa Nyuklia waIran.
Mazungumzo hayo yanaonesha hatua iliyopigwa katika mahusiano kati ya mataifa hayo mawili juu ya suala hilo.
Maafisa wanaoshiriki kwenye mazungumzo hayo hivi sasa wanalenga kutazama mambo muhimu zaidi ya mpango huo wa Iran, ambayo huenda yakatowa mwanga kuhusu ikiwa mazungumzo hayo yatafanikisha kupatikana makubaliano au la.
Mazungumzo ya kesho yanafuatia duru nyingine kadhaa zilizofanyika Rome na Muscat.