Duru ya mwisho ya hatua ya makundi CHAN kuanza leo Jumamosi
16 Agosti 2025Matangazo
Taifa Stars ambao tayari wako katika robo fainali, wanalenga kuweka historia ya kushinda mechi nne mfululizo katika CHAN. Katika mechi nyingine ya Kundi B, Madagascar watacheza dhidi ya Burkina Faso ambao tayari wameyaaga mashindano, katika dimba la Amani visiwani Zanzibar.
CHAN 2024: Harambee Stars yaishangaza Moroko
Madagascar lazima wapate ushindi ili kuyaweka hai matumaini ya kusonga mbele. Ni timu mbili tu za kwanza katika kila kundi zitakazojikatia tiketi ya kucheza hatua inayofuata ya robo fainali. Kufikia Jumanne jioni, timu nane zitakuwa zimethibitishwa rasmi.