DRESDEN:Mvutano wa kisiasa Ujerumani
1 Oktoba 2005Kansela Gerhard Scroder wa Ujerumani na mpinzani wake wa chama cha kihafidhina Angela Merkel wameshambuliana kwa maneno huku kila mmoja akimtaja mwenzake kuwa hafai kuingoza Ujerumani.
Hayo yametokea wakati vigogo hao wawili wa kisiasa wakiwa kwenye kampeini ya uchaguzi wa jimbo la Dresden ambao utafanyika hapo kesho jumapili.
Uchaguzi wa jimbo hilo haukufanyika kutokana na kifo cha mgombea.
Kansella Scroder amemshutumu Merkel kwa kukosa nguvu ya kusimama kidete kwa ajili ya mani iwapo viongozi wenye ubavu duniani watajaribu kuishinikiza Ujerumani kuingia vitani.
Kwa upande wake Merkel amesema serikali ya mseto ya chama cha Schroder cha SPD Na washirika wake wa chama cha walinda mazingira Grüne imeondolewa madarakani kwa kura na kwamba jambo hilo linajulikana kabla hata ya uchaguzi huu wa jimbo la Dresden na kansela atauona ukweli huo pole pole baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
Viongozi wote wawili wanamatumaini ya kujipatia kura katika uchaguzi wa Dresden ili kuimarisha misimamo yao wakati wa mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano mkuu baina ya vyama vyao ili kuweza kutekelza mageuzi muhimu nchini Ujerumani.
Viongozi hao wawili kila mmoja anataka kuwa Kansela.