DRESDEN:Matokeo ya mwisho ya Uchaguzi wa Ujerumani yatachelewa
9 Septemba 2005Matangazo
Kufuatia kifo cha mgombea mmoja wa uchaguzi mkuu ujao hapa ujerumani matokea ya mwisho ya uchaguzi huo huenda yakacheleweshwa.
Hatua hii inatokana na kusogezwa mbele tarehe ya uchaguzi katika eneo la Dresden ambapo wapiga kura watahitajika kusubiri hadi tarehe itakayotolewa.
Kwa mijibu wa sheria ya uchaguzi ya Ujerumani ,uchaguzi katika jimbo hilo utagombewa na mgombea mpya kwa niaba ya chama cha NPD.
Uchaguzi huo lazima ufanyike katika wiki sita za uchaguzi mkuu.
Maafisa wanasema uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba kura 220 za jimbo hilo huenda zikaamua mshindi katika matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu.