DRC yaukataa uteuzi wa kidiplomasia wa Kenya mjini Goma
17 Agosti 2025Matangazo
Tangazo la Kenya lilitolewa siku ya Ijumaa kama sehemu ya teuzi kadhaa za kidiplomasia.Wizara ya Mambo ya Nje ya Kongo imesema Kenya haikuwasiliana na serikali ya Kongo kabla ya kutoa tangazo hilo, kama inavyotakiwa na sheria za kimataifa na taratibu za kidiplomasia. Aidha imetoa wito wa tahadhari kwa hatua hiyo kutoonekana kama kile ilichokiita "kuhalalisha uvamizi haramu unaoendelea.M23, ni kati ya makundi karibu mia yanayopigana mashariki mwa Kongo, limejaribu kuanzisha serikali mbadala katika eneo hilo, ikidai kuwa inaikomboa kutoka kwa kile inachosema ni utawala mbovu kutoka Kinshasa.